Kanzi za Fasihi


Huu ni mkusanyiko unaoleta pamoja mawazo, hisia na fikra za waandishi mahiri kuhusu jamii. Ni juhudi za kuakisi ukweli wa hali halisi ilivyo na kumchorea msomaji taswira kamili kuhusu madhila ya uongozi, njaa, madawa ya kulevya na mahusiano ya kijamii; kwa ujumla yaliyodorora. Wakati huo huo, wanamzindua juu ya mabadiliko; kuu likiwa kupatikana kwa katiba mpya


Product Image Item Name-

Mimba ingali mimba na hadithi nyingine

Description

Author(s): Owen MacONyango

ISBN: 9966-01-059-9

Mimba Ingali Mimba na Hadithi Nyingine ni mkusanyo wa hadithi fupi uliofanywa kwa uangalifu mkubwa. Diwani hii imeleta pamoja hadithi fupi za aina tofauti kwa kuteua hadithi zenye mitindo na miundo mbalimbali. Ina maudhui yanayogusia matamanio, shida, fikra, falsafa kuhusu maisha, na vipengele vingi vya mazingira yanayoikumba jamii. Kupitia wahusika waliosawiriwa kwenye hadithi fupi zilizoko katika Mimba Ingali Mimba na Hadithi Nyingine, sherehe na milio ya waja inasimuliwa na waandishi stadi ambao wamenoa kalamu zao ili kuwasiliana na wasomaji kupitia nyanja hii ya fasihi.....

Ksh.340.00

Add:

 

Fahali Mtoboa Siri

Description

Author(s): Bitugi Matundura

ISBN: 9966-01-112-9

SIFA za jiji la Madongokuinama zilianza kupotea moja baada ya nyingine. Mito yake iliyokuwa na maji safi na baridi kama barafu ilianza kukauka. Misitu yake iliyokuwa na miti mbalimbali ilianza kushambuliwa ghafla na wanajiji walafi waliojinyakulia ardhi. Hatimaye kiangazi kilichoandamana na njaa kubwa kikatokea.....

Ksh.185.00

Add:

 

Maimuna

Description

Author(s): Rebecca Nandwa

ISBN: 9966-01-089- 0

Maimuna alikuwa na mazoea ya kula kila wakati. Muda si muda, mwili wake ukawa mkubwa kupita kiasi. Matatizo ya afya yakamwandama. Madaktari maarufu waliitwa lakini wakashindwa “kumtibu.” Mzee matambara alifanikiwa “kumponya” kwa kumpa masharti makali. Mwishowe Maimuna alibadilika na kuwa mrembo. Hadithi hii inawafunza wasomaji umuhimu wa kula vyakula bora wakati ufao, mazoezi ya viungo vya mwili na tabia njema.....

Ksh.150.00

Add:

 

Pango

Description

Author(s): K.W. Wamitila

ISBN: 9966-882-88-2

Pango ni tamthilia inayotufunulia na kujadili utata wa kisasa, uchumi, uongozi na migongano ya wimbi la kale na la usasa. Ni kichokozi na kichocheo cha fikra kwa wahakiki na wanafunzi vyuoni na katika shule za sekondari. Mwandishi ni mweledi wa lugha na kunga za fani ya tamthilia. Tamthilia hii ni mchango mwingine mwafaka katika medani ya fasihi hasa uga wa drama. Kwa mara nyingine tena, Wamitila amedhihirisha ukereketwa wake katika kuikuza na kuitilia mbolea fasihi ya Kiswahili hapa Afrika Mashariki. ....

Ksh.325.00

Add:

 

Mwongozo wa Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine

Description

Author(s): Timothy M. Arege, K.W. Wamitila, Deogratias Mwakyembe

ISBN: 9966-01-016-5

Mwongozo wa Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine unamwongoza msomaji kwenye vipengele vya kimsingi katika uchambuzi wa hadithi fupi. Waandishi wamezichambua hadithi zilizomo kitabuni kwa kuzingatia vipengele vya kimsingi kama dhamira na maudhui, muundo au msuko, tamathali za usemi na mbinu nyinginezo za kimtindo. Huu ni mwongozo ambao utamsaidia msomaji sio tu kuzielewa hadithi hizi vizuri bali pia kutambua maana zake zilizofichama.....

Ksh.180.00

Add:

 

Mwongozo wa Kifo Kisimani

Description

Author(s): Timothy M. Arege

ISBN: 9966-01-020-3

Mwongozo wa Kifo Kisimani unaichanganua tamthilia ya Kifo Kisimani kwa kuzingatia vipengele vya kimsingi vya tamthilia hii. Mbali na kuyachambua maudhui na tamthilia hii, mwandishi pia amevichanganua vipengele vya kifani katika misingi ya kidrama. Vipengele hivi ni pamoja na muundo, msuko, wahusika, kaida za kidrama, matumizi ya lugha na mbinu nyinginezo. Aidha kuna utangulizi unaovifafanua vipengele mbalimbali vya kidrama. Kitabu hiki kitawaongoza wanafunzi wa shule za upili na vyuo siyo tu katika kuielewa tamthilia ya Kifo Kisimani bali pia kupata msingi imara kuhusu uhakiki wa tamthilia.....

Ksh.180.00

Add:

 

Mwendo

Description

Author(s): Elieshi Lema

ISBN: 9966-01-084-X

Je, hujambo? Mambo ya huku Mtwara ni mengi mno. Siwezi kukueleza yote kwenye barua hii. Halafu tena naiandika kwa haraka shangazi asije akanikamata. Karatasi yenyewe nimeichomoa kwenye daftari la watu.....

Ksh.190.00

Add:

 

Msimamo Kamili

Description

Author(s): Francis Taylor

ISBN: 9966-882-57-X

Mtu yeyote anaweza kupatwa na UKIMWI. Wewe unaweza kupatwa na UKIMWI. Ili kuzuia ugonjwa wa UKIMWI usienee, ni lazima tuzungumze na tuzieleze habari za ugonjwa huu. Hii ndiyo sababu inayotufanya tuongee habari za UKIMWI sasa.....

Ksh.150.00

Add:

 

Kielezi cha Tungo

Description

Author(s): Timothy M. Arege

ISBN: 9966-01-096-3

Kielezi cha Tungo ni kitabu kinachojadili kwa mapana namna ya kuandika tungo mbalimbali. Hiki ni kitabu cha kipekee ambacho kimeangazia aina mbalimbali za tungo kwa kina. Mwandishi huyu anatoa mifano maridhawa katika kila utungo anaoushughulikia. Kina sehemu zinazoshughulikia maana na aina za insha, tungo amilifu, tungo za kifasihi, ufahamu na ufupisho. Aidha amelijadili kwa mapana swala la uakifishi. Kitabu hiki kitawafaa sana wanafunzi na walimu wa shule na vyuo mbalimbali pamoja na watu wanaokumbana na tungo za namna mbalimbali katika shughuli zao. ....

Ksh.450.00

Add:

 

Fasihi Andishi na Simulizi

Description

Author(s): P. I. Iribemwangi, Kariuki Chege & Betty Kiruja

ISBN: 9966-01-152-8

Fasihi Andishi na Simulizi ni kitabu kinachotalii fasihi hasa kwa kurejelea lugha ya Kiswahili. Kitabu hiki kinafafanua maana, jukumu na umuhimu wa fasihi. Hiki ni kitabu kinachouchanganua uwanja mzima wa fasihi ikiwa ni pamoja na kuchunguza fasihi andishi na pia fasihi simulizi. Juu ya hayo, hiki ni kitabu kinachochunguza mbinu mbalimbali za fasihi na mambo kama vile uhusika, msuko na ploti. Katika fasihi simulizi, waandishi wamechanganua tanzu tofautitofauti; kwa mfano, wameeleza aina mbalimbali za hadithi, ushairi simulizi, nyimbo na semi za aina tofauti. Vilevile, waandishi wamechunguza kwa kina tanzu za fasihi andishi kama vile riwaya, tamthilia, hadithi fupi na ushairi. Kwa kila mojawapo wa tanzu hizi, waandishi wametoa ufafanuzi uliokolea, kueleza mbinu za uchambuzi na kutoa mifano chungu nzima. Kitabu hiki kinatoa maelezo yenye kina kwa njia sahili inayoeleweka kwa urahisi. Mpangilio uliotumiwa unakifanya kitabu hiki kiwe na upekee wake. Kutokana na hayo, inadhihirika kwamba Fasihi Andishi na Simulizi ni kitabu muhimu cha rejea kinachoweza kutumika katika vyuo vikuu, vyuo na pia katika shule za upili. Ni kitabu muhimu kwa walimu wa Kiswahili na wapenzi wote wa fasihi na lugha ya Kiswahili.....

Ksh.0.00

Add: